Archive Page
1. Wawezeshaji lazima wajilinganishe na maudhui, falsafa na mkakati
wa Focus on the Family Familia (FOTF) – (Kuzingatia Familia).
Wawezeshaji wanatakiwa kufunzwa katika mtaala wa Hakuna Majuto® na kuidhinishwa
2. Wawezeshaji lazima wafuate msimamo wa sera ya FOTF kuhusu
masuala yafuatayo:
2.1 Ngono Kabla ya Ndoa
- Matendo ya kujamiiana kabla ya wakati yanaiharibu nafsi yako na nafsi za wengine.
- Uharibifu unaoletwa na shughuli za ngono za vijana ni pamoja na madhara ya muda mrefu ya afya na
ya mahusiano.
- Shughuli za ngono na watu ambao hawajafunga ndoa ni hatari hata bila kujali ni nani
uliyeshiriki naye.
- Kutoshiriki ngono hadi ndoa ni chaguo lenye afya bora kwa kila mtu.
2.2 Utoaji mimba
- Kwa mujibu wa thamani yetu ya msingi ya Utakatifu wa Maisha ya Mwanadamu: Tunaamini kwamba
maisha ya mwanadamu ni ya thamani na umuhimu usio na kifani katika nyanja zake zote, ikiwa
ni pamoja na watoto ambao hawajazaliwa, wazee, wajane, walemavu wa akili, wasiovutia, wenye
changamoto za mwili na kila hali nyingine ambayo inaonyesha uhai wa binadamu kutoka mimba
hadi kaburi.
2.3 Kuzuia mimba
- Kuzuia mimba ni vyema kuagizwa kama njia ya uzazi iliyokubaliwa kwa pande zote mbili katika
kuchelewesha kupata mimba ndani ya ndoa. Haipaswi kutambuliwa kama njia bora ya kuzuia mimba
katika kushiriki ngono kabla ya ndoa. Kwa kifupi, sio uthibitisho wa asilimia 100 kama njia salama ya
kuzuia mimba au magonjwa ya ngono, haswa katika kushiriki ngono kabla ya ndoa.
2.4 Kupiga punyeto
- acronymn FOTF inaona upigaji punyeto kuwa hauna madhara kiasili isipokuwa iwe tabia ya kupita kiasi
ambayo inaambatana na uraibu wa ponografia au inatumiwa tu kama njia ya kuridhisha utimilifu wa
ngono. Kupiga punyeto kunaweza pia kuleta athari mbaya za kijamii kwani kunaweza kuchukua nafasi
ya uhusiano mzuri na mtu wa jinsia tofauti kabla na baada ya ndoa
2.5 Ushoga na Ndoa za Jinsia Moja
- Ushoga ni suala tata, ambalo kwa jumla, ni chaguo la mtindo wa maisha kujihusisha na uhusiano wa
jinsia moja. Hakuna uthibitisho unaotegemeka na wa uhakika kwamba ushoga ni tabia mtu amezaliwa
nayo au umepangwa wakati wa kuzaliwa (kijeni). Kuwasaidia na kuwaelewa wale wanaopambana na
ushoga limebakia kuwa ni jambo la msingi linalotuletea wasiwasi.
- Tunaamini kwamba ndoa inategemea ukweli wa kibiolojia kwamba uzazi unategemea mwanamume na
mwanamke, na ukweli kwamba watoto wanahitaji mama na baba. Tunaamini kwamba ndoa ni msingi wa
ustaarabu wote wa binadamu, na inawaleta pamoja wenzi wanaokamilishana kingono, katika uhusiano
wa mke mmoja, ambapo wanaahidiana kuwa waaminifu kwa viapo vya kudumu na kutengwa.
3. Wawezeshaji hawapaswi kubinafsisha maudhui ya mazungumzo.
4. Ili kujiwakilisha wenyewe na FOTF (Zingatia Familia) vyema,
wawezeshaji wanapaswa kuwa wamevalia vizuri ipasavyo na nadhifu.
- Pitia kwa kina mtaala wa Hakuna Majuto® .
- Itakuwa vyema kuwasilisha nyenzo katika timu za angalau watu wawili, kila mmoja akizingatia kusoma masomo mawili ama nusu ya kila somo.
- Badilisha mawasilisho yako baada ya kufahamu sehemu yako kwa kina.
- Fanya mazoezi na wenzako, ukizingatia muda wa mawasilisho.
- Mwambie mtu akuangalie na akukosoe wakati unapofanya mawasilisho.
Sifa 3 za mshirikishi mwenye ufanisi
Kushirikisha/Kujumuisha
Changamsha – utakuwa unazungumzia masuala ya kibinafsi. Tulia uwe muwazi - tumia hadithi na mifano yenye nguvu! Uweze kufikiria umri wa wasikilizaji wako, hatua ya maisha waliyopo:
Kwa vijana wadogo (Wanafunzi wa sekondari za chini)
- Wakati wote fafanua maneno magumu au ya kiufundi na uepuke kutumia lugha iliyorembwa.
- Tumia mifano na hadithi kueleza hoja zako. Kwa mfano, matukio ya kawaida kutoka kwa programu za TV au uzoefu halisi wa maisha.
- Hakuna haja ya kutoa maelezo mengi sana inapokuja kwa mifano au hadithi zinazohusiana na ujinsia. Toa hoja katika kauli moja au mbili fupi.
- Huenda ukahitaji kuwasaidia kuelewa baadhi ya mabadiliko ya kimwili na ya kihisia ambayo wanayapitia wakati wa kubalehe.
Kwa vijana wakubwa (Wanafunzi wa sekondari za juu)
- Tumia sauti ya kimahusiano zaidi na jizuie kuongea na wanafunzi kama kwamba hawana ujuzi.
- Tumia hadithi za kibinafsi kadiri uwezavyo ili kuanzisha maelewano na wasikilizaji wako.
- Unaposhiriki mfano au hadithi inayohusiana na ngono, kumbuka kushiriki maelezo ya kutosha ili kueleza hoja, lakini usishiriki maelezo ya picha ya ngono au ya wazi, ambayo yanaweza kuibua udadisi wa wanafunzi au kuwasumbua
- Ukiulizwa na wanafunzi, usitoe taarifa zaidi ya inavyotakiwa, hasa katika eneo la kujamiiana. Kwa
mfano, ikiwa swali ni “Ponografia laini ni nini?”, lishughulikie kwa ufupi na endelea na uwasilishaji. Usitoe habari zaidi, tuseme, kuhusu aina zingine za ponografia, ambayo iko nje ya upeo wa swali lililoulizwa.
- Hii ni hatua katika maisha yao ambapo wanajaribu kujitambua na kupitia masuala ya urafiki, kwa hivyo mbinu inapaswa kulenga kuwasaidia kujitambua kwamba kila mmjoa wao ni mtu wa kipekee.
- Katika hatua hii, bado wanakuza namna ya kufanya maamuzi kikamilifu. Ni muhimu kuwasaidia kufikiria juu ya maamuzi yao na kuwaongoza ili wafanye maamuzi bora.
Ngazi ya chuo kikuu (Wanafunzi wa baada ya sekondari)
- Vijana katika hatua hii wana uwezo bora wa kuchanganua na kuchuja ujumbe. Thibitisha maoni tofauti na uwape changamoto kufanya uamuzi bora zaidi.
- Tumia mifano halisi ya watu wa umri wao na mifano ya jinsi ya kudumisha uhusiano mzuri na watu wa jinsia tofauti katika eneo la uchumba.
- Katika eneo la kujamiiana, kumbuka kushiriki maelezo muhimu na ya msaada pekee, na kuacha
maelezo ya wazi ya kingono yasiyo ya lazima, ambayo yanaweza kuibua udadisi wa wanafunzi
au kuwasumbua.
- Vijana katika hatua hii wanaweza kutaka kuchunguza zaidi na kujua zaidi kuhusu eneo fulani la ujinsia.
Ikiwa watauliza swali, waelekeze wakwambie kile wanachofikiria, ili kuwapa changamoto ya kupata
majibu machache toka kwao. Chukua majibu yao na kuyatumia kuwaongoza kwenye mwelekeo mzuri.
Mtazamo mwema
Mtazamo wako utakusaidia kuwashawishi na pia kuthibiti majibu utakayopata kutoka kwa hadhira.
- Uwazi – unahimiza uaminifu kupita toni ya sauti yako na unavyowatazama usoni.
- Uchangamfu – unawavutia na hasa ikiwa kwa dhati uchangamfu unatoka moyoni.
- Furahia –jenga mazingira mazuri kupitia lugha ya mwili (jinsi unavyojiwasilisha mbele yao).
- Upendo – unawasilisha huruma na kuonyesha kuwa unawapenda wanafunzi.
- Mamlaka – wafanye wahisi wana ujasiri kupitia sauti yako na mapozi yako.
Mawasiliano mwafaka
Sekunde 15 za kwanza za ufunguzi wako ni muhimu. Dhana ya wengi kwenye hadhira yako hujengwa
wakati huu, kutokana na kile wanachokiona. Hivyo jinsi unavyosimama, kile ulichovalia na jinsi
unavyotembea ni muhimu sana.
Mwasilishaji mzuri ni yule ambaye:
- Anawakilisha tabia nzuri, uadilifu na unyenyekevu.
- Mchangamfu, anayeelewa na anayeweza kufikiwa kwa wepesi.
- Yuko tayari kushiriki vipengele vya maisha yake na kikundi.
- Anashughulikia kila mmoja kwa heshima na uadilifu.
- Hawalazimishi watu kusema ama kushiriki katika hali ambazo hawataki bali anajenga hali ambayo
inawafanya watake kushiriki.
- Anawasaidia watu kuwasiliana wao kwa wao.
- Anaamini kuwa kila mtu kwenye kikundi ana maoni yanayostahili kusikilizwa.
- Ana subira ya kuwavutia watu na kuwasaidia kueleza maoni yao.
- Ni msikilizaji mzuri anayehimiza watu kusikiliza kwa heshima kile kinachosemwa.
- Hajitakii makuu, lakini anazingatia maslahi ya watu kwenye kikundi.
- Hana ugumu, lakini anaweza akayasikia mawazo ya watu kwenye kundi.
- Anaepuka kuwa mkosoaji au mwenye msimamo mkali kwa washiriki.
- Hatarajii kuwa mshirikishi mkamilifu lakini yuko tayari kujifunza kutokana na uzoefu.
- Anaweza kufunzika na ana jaribu kujenga kanuni za msingi za mawasiliano mema
Pitia orodha hii tena na uweke alama kwenye hoja ambazo umefuza vyema kwa sasa. Zile ambazo
hukuziwekea alama zishughulikie unapofunza kwenye warsha ijayo.
Kudumisha uchangamfu na mazingira ambayo kila mmoja anaweza kushiriki:
- Mjadala uwe na malengo.
- Panga viti vya washiriki kwa njia ambayo kila mmoja atakuona wakati wa mjadala. Iwapo itawezekana
washiriki wakae kwenye vikundi vya watu wanne hadi sita. Waite washiriki ukitumia majina yao ya
kwanza (tumia vibandiko vya majina yao), kila mmoja ashiriki.
- Sisitiza hoja muhimu na uache waulize maswali.
- Chunguza kila mshiriki, wambie watoe maoni yao kwa viwango vya uelewaji wao.
- Fahamu hulka ya kila mshiriki na uwajumuishe wale viherehere kwenye vikundi.
Makosa 10 ya Mshirikishi
1. Maandalizi mabaya – kusahau nakala zako, mtaala au vifaa, kuchelewa n.k
2. Kumwaibisha mshiriki ili achekwe.
3. Kutozungumza na chumba kizima.
4. Kushindwa kuthibiti kikundi.
5. Kutumia muda mwingi kwa mada zisizohusiana.
6. Kufundisha bila kuwajumuisha ama kuwashirikisha washiriki.
7. Kukosa kuwashirikisha hadithi yako ama uzoefu wako.
8. Kutoangalia muda na kupitiliza muda uliowekwa.
9. Kutovaa kiheshima au ipasavyo.
10. Kukosa kufanya utathmini baada ya warsha kukamilika
Maswali ni ishara nzuri kuwa washiriki wamevutiwa na kile unachosema. Unapoyajibu, yajibu kana kwamba ni mazungumzo ya ana kwa ana, huku wengine kundi zima wakisikiliza.
Tarajia maswali. Jifunze jinsi ya kudhibiti vipindi vya maswali na majibu kwa urahisi na unyenyekevu. Tengeneza majibu yako ukitumia yale yaliyomo kwenye mwongozo ama mtaala huu ukikariri hoja zilizomo. Ukifanya mazoezi na kujiandaa vya kutosha unaweza ukajibu maswali mengi ambayo yataulizwa kwenye warsha. (ama kwenye mazungumzo na mwanao wa kike ama kiume).
“Neno lililosemwa wakati unaofaa ni kama matofaa ya dhahabu kwenye sahani ya fedha. Ni kama hereni ya dhahabu ama pambo la dhahabu safi ndivyo alivyo mwonyaji mwenye busara
kwa sikio linalosikia.”
– Ancient Proverb
Mambo 11 muhimu ya kukumbuka
1. Hakuna maswali ya ujinga, ila tu majibu ya ujinga.
Majibu yako ya busara yatakabiliana na majibu ya ujinga ya vijana wanayoyasikia kutoka kwa vyombo vya habari, kutoka kwa vijana wenzao na vipindi vingine ambavyo si vya manufaa kwao.
Maswali ndio wakati wa maneno ya hekima, uponyaji na kuwatia moyo. Majibu yako kwa swali
hayasikilizwi tu na yule aliyeuliza bali yanasikilizwa na wote wanaoshiriki. Maneno yana nguvu
– kisaikolojia na pia kihisia. Yanaweza kufahamisha, kuumiza ama kuponya. Maneno yanaweza kuleta matumaini.
Washiriki wako wanaweza kuwa wanauliza jambo ambalo ni gumu kulielezea. Sikiliza kwa masikio,
ubongo na moyo. Unaposikiliza kwa makini, chuja kila swali ili uweze kufikia kina cha suala hilo. Huu ni wakati wako wa kuwa mjumbe wa matumaini na uponyaji.
2. Sio maswali yote yanayohitaji majibu.
Mara nyingi kutakuwa na yamkini kijana mmoja kwenye kundi ambaye atakuwa akitaka kukujaribu.
Swali hili mara nyingi ni la moja kwa moja na linaaibisha na hata huenda likafanya sura yako ikabadilika.
Huenda aliyeuliza anataka washiriki wacheke. Swali pia linaweza kuelekea kwenye maudhui yenye ubishani au kukutaka ufichue maelezo yasiyofaa umri wa kundi hilo. Pumua kwa kirefu na usijibu mara moja mbele ya kundi lote. Badala yake chagua mojawapo ya majibu haya:
- “Hilo linaonekana kama swali la kibinafsi. Waonaje iwapo tunaweza kukutana baada ya somo
hili na kujadili kando na saa za warsha au kujadili hilo na mshauri wako wa shule?”
- “Samahani, lakini swali hilo si la heshima kwa washiriki wengine. Swali jingine, tafadhali.”
3. Sio maswali yote yanapaswa kujibiwa nawe
Waelekeze vijana kwa wazazi wao, walimu ama watu wazima wanaoaminika. Iwapo majibu yamo kwenye nyenzo ambazo tayari umezishughulikia au utazishughulikia, jaribu kulirejesha kwa vijana walijibu:
- “Ninyi mnafikiriaje? Je, kuna yeyote hapa ambaye angependa kujaribu kulijibu?”
- “Swali zuri! Fikiria jinsi ungelijibu swali hilo, kwa sababu baadaye hilo ndilo tutakalo kuwa tunajifunza.”
Iwapo kijana atakosea jibu , una nafasi nzuri ya kufundisha dhana hiyo tena.
4. Huhitaji kufahamu kila jibu la kila swali litakoloulizwa.
Usiwe na hofu ya kusema, “Sijui jawabu la swali hilo.” Iwapo ni sawa, nitaleta ama nitakujibu wakati
mwingine tutakapokutana.
Iwapo utaulizwa swali gumu, likubali, kisha pata jina la mtu aliyeuliza na uahidi kulijibu baadaye:
- “La haula! Hilo ni gumu! Wacha nitafakari kisha nitalirejelea baadaye.”
- “Swali zuri! Je, kuna yeyote hapa angependa kujaribu kulijibu?”
- “Wacha nione iwapo nilikuelewa vizuri? Je, wote mmesikia swali hilo?” (Kisha uliza kwa
maneno mengine.)
- “Je, waweza ukarudia hilo swali tena?”
- “Nahitaji kufikiria kuhusu hilo kwa muda. Nitajaribu kulijibu baadaye/kesho.” (Kisha kumbuka kulijibu.)
Unaweza ukaulizwa swali ambalo linasababisha kicheko. Huenda ukacheka hata wewe. Iwapo hujajiandaa
unaweza ukasema hivi:
- “Hilo ni swali ambalo ningependa kujibu wakati wa mapumziko mafupi.” (hatua hiyo itasaidia kuondoa
shinikizo la kujibu swali la kunata mbele ya kundi zima. Wakati mwingine huenda aliyeuliza anataka
kukuaibisha. –usiache hilo lifanyike mbele ya kila mtu.)
- “Swali zuri, lakini ningependa kufikiria kuhusu jawabu lake kiasi. Wacha tulirejelee kabla sijaondoka”
ama, “tutalirejelea kesho.” (Hakikisha kuwa utalirejelea.)
- “Ahsante kwa ujasiri wa kuuliza swali hilo; Yafuatayo ni baadhi ya mawazo kuhusu hilo...”
5. Tumia fursa hiyo kufundisha kanuni nzuri.
Chora taswira ama picha ambayo vijana watakumbuka. Maswali mengi yatatumika kutoa fursa ya
kutafakari na kufundisha tena dhana hiyo. Tumia vifaa na miongozo ambazo tayari imeishafundishwa ili
kuwasaidia vijana kuweza kusisitiza ukweli katika bongo zao.
6. Chukua muda wa kujibu swali kwa umakinifu.
Unapotaka kutumia maneno yaleyale, usiogope kutumia maandishi kwenye nakala yako ama mwongozo
wa mkufunzi. Utakuwa unawafunza vijana kuwa unapotaka kupata jibu mwafaka na sahihi, unatafuta
chanzo cha habari hizo.
7. Punguza idadi ya maswali utakayojibu.
Sema kitu kama, “Tuna muda wa maswali matatu.”
8. Hakikisha kuwa washiriki wanauliza maswali.
Muda mwingi unaweza ukatumiwa kutoa maoni, ambayo huenda yakawachanganya washiriki wengine.
Iwapo hili litafanyika, taratibu ingilia kati na useme, “Samahani, lakini kwa sababu ya wakati, unaweza
kufafanua swali lako, tafadhali?”
9. Use question cards (or Slido.com).
Waelekeze washiriki kuandika maswali wanapofikiria na kuyatumbukiza kwenye sanduku la maoni ambalo
liko kwenye chumba. Tazama ndani ya sanduko hilo wakati wa mapumziko na uchague kati ya maswali
yaliyomo kwenye sanduku ili uyajibu. Hii itamsaidia kijana mwoga na pia kumpa ujasiri yeye ambaye
hataki kuuliza swali mbele ya wengine.
Usiwatangaze wale ambao hawangependa kutambulika wakati wanapotaka kuuliza maswali kwa njia ya siri.
Iwapo swali litaendelea kuulizwa na washiriki wengi, lijumuishe kwenye wasilisho lako.
10. Uliza maswali.
Uliza maswali ambayo huibuka kwenye warsha nyingine. Huenda washiriki wakawa na swali moja lakini
wasiwe na ujasiri wa kuuliza mbele ya wengine.
11. Shirikisha yale ambayo ni ya manufaa na epuka yasiyofaa.
Shiriki tu kile kinachohitajika na kusaidia, haswa linapokuja suala la mada juu ya ujinsia. Unaposhiriki
mfano au hadithi yako mwenyewe, toa maelezo ya kutosha ili kueleza jambo kuu na uepuke kutoa
maelezo ambayo ni ya ziada, kwa mfano, maelezo ya picha ya ngono ambayo yanaweza kuibua udadisi
wa vijana kwa njia isiyofaa au kuwasababishia usumbufu. Isipokuwa ukiulizwa, usitoe habari zaidi kuliko
inavyohitajika. Na hata wakati kijana anataka kuchunguza zaidi, elekeza upya au urejeshe swali ikiwa
unahisi litaingia katika maudhui yenye ubishi. Inapobidi, unaweza kueleza kuwa hutajibu swali kabisa au
wakati wa warsha (rejea nukta 2).